Mahitaji
- Nyama nusu kilo
- Papai mbichi
- Tangawizi mbichi
- Limao 2
- Ndizi 3
- Chumvi kiasi
Kuandaa
- Katakata nyama vipande vidogo,nyama iwe nundu tafadhali
- Ponda tangawizi weka kwenye nyama
- Kamulia malimao
- Fefenya chumvi
- Katakata papai na weka kwenye nyama
- Vichanganye na vifunike viache kwa nusu saa
- Washa moto kama unatumia mkaa
- Chomeka nyama kwenye chuma au stick(zipo special kwenye supermarkets)
- Anza kuchoma hadi ziwe ukaa
- Menya ndizi na ziweke motoni zigeuze zikiiva utaona zimekuwa ngumu
- Andaa sahani weka mishkaki yako na ndizi na matango/pilipili au kashumbari kama unapenda
Maisha Furaha!
No comments:
Post a Comment